Home > CCM > Nataka nafasi kama ya Kinana, CCM – Rama Dee

Nataka nafasi kama ya Kinana, CCM – Rama Dee

Msanii wa muziki wa R&B, Rama Dee amedai kama akiingia kwenye uongozi basi anataka nafasi za juu huku akiitolea mfano nafasi ya Abdulrahman Kinana ya Ukatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kipenda Roho’ amedai hataki nafasi ndogo ndogo ambazo kila mtu anaweza kuipata kama akiamua.

“Nitagombea ubunge mimi?, mimi nataka kuwa juu ya watu, napenda nafasi kama ya Kinana, nataka nafasi kubwa, kama katibu mkuu wa chama,” Rama Dee alimjibu mmoja ya mashabiki wake ndani ya Kikaangoni cha EATV.

Pia alisema Mh Rais  Magufuli akiamua kumteua  nafasi ya Uwaziri atakubali kwa sababu hawezi kukataa kazi aliyopewa na rais wa nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *