Home > Bunge > Prof. Kabudi awasilisha cheti UDSM kwa uhakiki

Prof. Kabudi awasilisha cheti UDSM kwa uhakiki

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema tayari amewasilisha cheti cha kidato cha nne katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa ajili ya kupelekwa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) kwa ajili ya uhakiki.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi mjini Dodoma jana, Profesa Kabudi alisema cheti hicho alikuwa ameshakiwasilisha kwa uhakiki lakini hajui ilitokea nini hadi ikaonekana hakipo.

“Yaliyotokea huko siyajui na hayanihusu, ila unachoweza kuandika ni kwamba nimeshawasilisha cheti changu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wao watakipeleka kwa Necta kwa uhakiki,” alisema.

Jina la Profesa Kabudi limetokea katika orodha ya watumishi wa UDSM ambao vyeti vyao havikukamilika kwa uhakiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *