Home > CCM > Kambi,Mafunzo Kwa Vijana Wa Vyuo Na Vyuo Vikuu UVCCM Yamalizika Hombolo.

Kambi,Mafunzo Kwa Vijana Wa Vyuo Na Vyuo Vikuu UVCCM Yamalizika Hombolo.

Na: Mwandishi wetu, Dodoma.
Wanafunzi kutoka vyuo 10 vya Mjini Dodoma wamemaliza Kambi/Mafunzo ya siku tatu(3) yaliyotolewa kwa Lengo la kuwaongezea Ufahamu juu ya Chama Cha Mapinduzi na Mambo mbalimbali yanayoendela hapa nchini.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa 23/06/2017 na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole na kufungwa 25/06/2017 na Katibu wa NEC siasa na uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga yalihusisha wajumbe 551 wa Vyuo na Vyuo Vikuu vilivyopo katika Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza wakati wakati wa Kambi/Mafunzo hayo Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela alisema Serikali ya Awamu ya tano(5) imejiandaa kikamilifu kikamilifu kupambana na Wezi wa mali za Umma.
“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imejipanga katika kuzuia mianya yote ya rushwa, nasisitiza kuwa hakuna mwizi atakayesalia katika ujenzi wa CCM Mpya na Tanzania mpya” Alisema Ndg. Lubinga.

Pia akizungumza baada ya kufungwa mafunzo hayo Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na vyuo vikuu UVCCM Ndg. Daniel Zenda alisema kambi imeisha salama na vijana wameyapokea vizuri mafunzo hayo.
“Tunamshukuru mungu tumemaliza salama kambi/ mafunzo yetu na vijana wameyapokea vizuri na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote waliyofundishwa sambamba na kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kwa yale yote anayoyafanya” alisema Kaimu Katibu wa Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM.

Pamoja na hatua aliyochukua Rais Magufuli juu ya kuzuia kusafirisha mchanga wa madini inapaswa kuungwa mkono na watanzania wote kwani pesa hizo zingesaidia kufanya shughuli nyingi za Maendeleo kama kuwezesha vijana kupata mikopo kupitia vikundi na Mikopo ya elimu ya juu, ujenzi wa Madarasa, Mabweni, Hospitali na Nyumba za walimu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo waliwataka wawe wazalendo kwa nchi yetu sambamba na kumuunga mkono Rais Magufuli kwa yale anayoyafanya ya kuwatetea wananchi wa Tanzania hususani Maskini na wanyonge. Dhamira na hatua anazochukua tunaziona kwa Vitendo ni dhahiri na ni shairi. “Maana Uzalendo ni Vitendo”.

Wakati huo huo baada ya kumaliza mafunzo hayo Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lupinga aliweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Ofisi ya Vyuo na Vyuo Vikuu Tawi la Hombolo.

Baadhi ya wana Vyuo na Vyuo Vikuu wakifuatilia mafunzo hayo.
Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na vyuo vikuu UVCCM Ndg. Daniel Zenda alizungumza katika mafunzo hayo.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lupinga akizungumza katika mafunzo hayo ya wana Vyuo na Vyuo Vikuu Dodoma.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lupinga akiweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Ofisi ya Vyuo na Vyuo Vikuu Tawi la Hombolo.
Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole akitoa mafunzo kwa Vijana wa Vyuo na vyuo vikuu mjini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *