Home > Featured_Slider > NIDA Yaibuka Kidedea Maonyesho Ya 41 Ya Kimataifa Ya Sabasaba 2017.

NIDA Yaibuka Kidedea Maonyesho Ya 41 Ya Kimataifa Ya Sabasaba 2017.

Mamlaka ya Vitambusho vya Taifa (NIDA) imekuwa moja ya Taasisi zilizofanya vizuri katika maonyesho ya Sabasaba mwaka huu kwa kupata tuzo ya Banda Bora katika kundi la Wizara za Serikali na Taasisi “Best Exhibitor Government Ministries & Agencies” kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 41 Sabasaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Dar-es-salaam. Takribani kampuni za Ndani 2500 zikiwemo Wizara na Taasisi za Serikali zinashiriki maonyesho hayo, pamoja na kampuni za kigeni 500 zinazowakilisha Nchi 30 duniani.

 

Maonyesho hayo yaliyoanza Tarehe 28 June 2017 yanatazamiwa kumalizika Julai 13, 2017. Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) katika maonyesho ya mwaka huu imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwa wananchi zinazohusu Utambuzi na Usajili wa Watu  ikiwemo huduma ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa na uchukuaji alama za Kibailojia, kusaidia wananchi waliokwisha sajiliwa na hawajapata vitambulisho vyao, kujua hatua za Maombi yao pamoja na kutoa Elimu kwa umma kuhusu faida, umuhimu na matumizi mapana ya Kitambusho cha Taifa katika ukuzaji Biashara na maendeleo ya Viwanda sambamba na kauli mbiu ya Maonyesho hayo “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda.

 

NIDA imehakikisha ushiriki wao katika Maadhimisho ya mwaka huu unaendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu” kwa kuhakikisha wananchi wanaosajiliwa katika siku 13 za maonyesho hayo wanapata Vitambulisho vyao ndani ya siku hizo.

 

3
Baadhi ya Watumishi wa NIDA walioshiriki kufanikisha Maonyesho hayo wakiwa na nyuso za furaha baada ya kupokea Tuzo ya ushindi. Kutoka kulia ni Edna Wanna, akifuatiwa na Agnes Gerrald, Raymondn Sengate na Sarah Mashalla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *