Home > Featured_Slider > Mkuu Wa Wilaya Ya Arusha Atoa Msaada Kwa Walemavu Wa Jiji La Arusha.

Mkuu Wa Wilaya Ya Arusha Atoa Msaada Kwa Walemavu Wa Jiji La Arusha.

Serikali ya Wilaya ya Arusha imetoa msaada wa Baiskeli 50 kwa walemavu wa Jiji la Arusha(Kila Kata Baiskeli 2). 

Baiskeli hizo zimetolewa jana tarehe 08/07/2017 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw Gabriel Daqqaro akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya Bw David Mwakiposa,Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Anna Mwambene,Rais wa Wheeel Chair Duniani Bw David Behring, Mratibu wa Conservation Foundation of Tanzania Bw Gerald Kazungu na watendaji Kata zote 25 za Jiji la Arusha. Msaada umekuja miezi sita tu tangu Serikali ilipotoa mikopo isiyo na riba ya pikipiki 200 zenye thamani ya milioni 400 kwa Vijana wa Jiji hilo.

Aidha, Kuanzia mwisho mwezi huu Julai 2017, Serikali ya Wilaya hiyo itaanza kutoa mikopo ya Sh Milioni 100.Hii ni mikopo isiyo na riba kwa akina mama 500 (20 kila Kata) kila mmoja atapata Sh 200,000 ili kuwakwamua kiuchumi na kuwasaidia kuendelezaa biashara zao. Mikopo hii ni nje ya 10% ya fedha zitolewazo na Halmashauri ya Jiji kwa vijana na wanawake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *