Home > Featured_Slider > Ngeleja Akubali Kurudisha Pesa Za ESCROW.

Ngeleja Akubali Kurudisha Pesa Za ESCROW.

Mbunge wa Sengerema Mhe. William Maganga Ngeleja amesema yuko tayari kurudisha pesa alizopewa na mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow ndugu James Lugemarila ambaye ni mmiliki wa kampuni ya VIP engineering and marketing limited.Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo mbunge huyo amesema alizipokea fedha hizo 12/2/2014 kupitia benki ya MKOMBO ambapo ziliingizwa katika akaunti yake ya 001101102352601.

Ngeleja amesisitiza kuwa fedha hizo alizipokea kwa nia njema ikiwa ni kwa ajili ya kumsaidia katika shughuli zake za kibunge hususani kusaidia wananchi wa jimbo lake la Sengerema na taifa kwa ujumla.Kutekeleza shughuli za kijamii mfano ujenzi wa makanisa,misikiti, kulipia karo za wanafunzi wasiojiweza na kadharika.Na shughuli za maendeleo ambazo hazipo kwenye bajeti ya serikali.Nilipokea fedha hizo toka kwa ndugu Rugemalira bila kujua kuwa ni pesa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya fedha ya Tegeta Escrow kama ilivyo sasa,amesema Ngeleja.

Mbunge huyo amesema baada ya kupokea msaada huo alifuata tararibu zote ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwenye sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma 24/12/2014 na 15/01/2015 alilipa kodi kwa mamlaka ya mapato Tanzania kiasi cha 13,238,125Mil ikiwa ni 30% ya msaada huo aliopewa kama ilivyoelekezwa na Nilipokea fedha hizo kama wapokeavyo wabunge wengine kwa nia njema,bila kujua kwamba James Rugemalira baadae angekuja kuhusishwa na kashfa ya fedha za akaunti ya Tegeta Escrow kama ilivyo sasa.

Kwa vile sasa imethibitika rasmi kuwa aliyenipa fedha hizi anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunt ya Escrow,nimepima na kutafakari na hatimaye kuamua kwa hiyari kurejesha serikalini (TRA) fedha zote nilizopewa kama msaada (TSH 40.4M) bila kujali kuwa zilishakatwa kodi ya mapato kama nilivyoeleza hapo juu,amesema mheshimiwa Ngeleja huku akiwaonyesha wanahabari risti ya malipo ya fedha .Ngeleja ameongeza kuwa ameamua kurudisha fedha hizo hata kama aliyempa bado ni mtuhumiwa tu na hajapatikana na hatia kwa sababu hataki kuwa sehemu ya tuhuma ama kashfa hiyo tena.

“Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa umma,na pia niliwahi kuitumikia wizara ya Nishati na madini kwa takribani miaka mitano na nusu nikiwa kama naibu waziri na hatimaye waziri kamili lakini sikuwahi kukumbwa na kashfa ya rushwa na ufisadi hivyo nimesononeka a kufadhaika sana kuona kuwa msaada niliopewa sasa unahusishwa na tuhuma amesisitiza mbunge huyo.

Pia Ngeleja amesema anarudisha fedha hizo kulinda heshima na maslahi mapana ya nchi yake,chama chake,serikali na wananchi wake wa jimbo la Sengerema na familia yake na yeye binafsi.Pia Mheshimiwa Ngeleja amempongeza rais John Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya na kusema anamuunga mkono kwa juhudi zake zote za kuliletea taifa maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *