Home > Featured_Slider > BODI TPSC YAAGIZWA KUSIMAMIA UTOAJI WA ELIMU BORA KWA WATUMISHI WA UMMA

BODI TPSC YAAGIZWA KUSIMAMIA UTOAJI WA ELIMU BORA KWA WATUMISHI WA UMMA

Bodi ya ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) imetakiwa kuhakikisha inaimarisha utoaji wa elimu bora na yenye viwango kwa watumishi wa umma ili kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotaka watumishi wenye weledi na wenye maadili katika sekta za umma na binafsi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki alipokuwa akizindua Bodi ya washauri wa chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.

Waziri Kairuki ameeleza kuwa ni wakati sasa kwa chuo hicho kuwa mfano bora wa kutoa watumishi ambao watarejesha nidhamu, utumishi bora na uadilifu wa hali ya juu katika sekta za umma na binafsi ili kumaliza tatizo la watumishi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo viovu kama rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.
“Chuo cha utumishi wa umma hapa nchini kilianzishwa kwa lengo la kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma, hivyo Bodi ya ushauri wa chuo cha utumishi wa umma wa Tanzania inalo jukumu la kuhakikisha kuwa lengo hili linatekelezwa kwa ufanisi mkubwa,” alisema Waziri Kairuki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *