Home > Habari mchanganyiko > Hukumu Ya Mahakama Kesi Ya Kutumia Dawa Za Kulevya Ya Manji.

Hukumu Ya Mahakama Kesi Ya Kutumia Dawa Za Kulevya Ya Manji.

Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 6, 2017 imetoa hukumu katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya iliyokuwa ikimkabili mfanyabishara Yusuf Manji.

Hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha ambapo mfanyabishara huyo sasa yupo huru.

Mahakama hiyo imemuachia huru Yusuf Manji baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kosa la matumizi ya dawa za kulevya.

Yusuf Manji alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akituhumiwa kwamba, kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View, Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine.

Manji ambaye alikuwa mshtakiwa alikuwa na mshahidi 7 wakati upande wa mashtaka ulikuwa na mshahidi watatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *