Home > Featured_Slider > SABA WANUSURIKA KIFO BAADA YA GARI WALIYOPANDA KUGONGA TRENI JIJINI TANGA

SABA WANUSURIKA KIFO BAADA YA GARI WALIYOPANDA KUGONGA TRENI JIJINI TANGA

Watu saba wamenusurika kifo huku wawili  wakijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo baada ya gari ndogo waliokuwa wamepanda aina ya Carry kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ya Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda, gari hilo baada ya kufika eneo la makutano ya reli wakati likijaribu kusimama  lilifeli breki na kuiparamia treni hiyo.

Ajali hiyo ambayo ilitokea jana eneo la makutano ya reli Kwaminchi Jijini  Tanga iliacha mshangao mkubwa kutokana na mazingira ya namna ilivyotoke ambapo gari ndogo ilikuwa ikitokea eneo la Kwaminchi.

Akithibitisha kutokea tukio hilo jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba alisema ajali hiyo ilitokea saa kumi jioni katika eneo hilo ambapo gari hilo ilifeli breki na kuparamia mabehewa ya reli wakati ikipita katika eneo hilo.

Aliitaja gari hiyo aina ya Carry ambayo ilipata ajali hiyo kuwa ni T.343 DCQ  iliacha njia na kuigonga treli iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuingia  kwenye stesheni ya Tanga.

Aidha alisema majeruhi sana waliokuwepo kwenye ajali hiyo walifikishwa  kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu zaidi huku Dereva wa gari hilo akitokomea.

Kamanda huyo alisema kutokana na kukimbia kwa dereva huyo wataendelea kumsaka ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kamanda huyo alitoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha kwenye maeneo ya kivuko cha reli wanakaa mita 50.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *