Home > Bunge > SERIKALI YAIONYA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI NA MBUNGE ZITTO KABWE

SERIKALI YAIONYA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI NA MBUNGE ZITTO KABWE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika ameionya Manispaa ya Kigoma- Ujiji pamoja na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuacha mara moja mawasiliano na ushirika wa ‘Open Government partinership (OGP)’ na kama ikiendelea kufanya hivyo basi itachukuliwa hatua kali.
“Nataka niionye Manispaa ya Kigoma waache mara moja, watekeleze maamuzi ya serikali, na wakiendelea kufanya mawasiliano kama wanavyofanya sasa serikali itachukua hatua kali zaidi,” amesema Waziri Mkuchika.

Waziri Mkuchika ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali mawili ya nyongeza yaliyoulizwa na Mbunge Zitto Kabwe Bungeni na mojawapo likiwa ni Serikali inatoa kauli gani kuhusiana na ushiriki wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na miji mingine inayotaka kuingia katika OGP.
“Andiko la OGP linasema kuwa nchi ikijitoa, basi na wanachama wake wote walioko ndani ya ile nchi shughuli zao zinakoma,” alisema Mkuchika.

Aidha Waziri Mkuchika alieleza kuwa kujitoa kwa Tanzania katika OGP, hakukufanywa kwa kumuiga mtu bali kwa kupima vigezo ambavyo iliviona vinafaa kwani ni taifa huru linalojitawala na kufanya maamuzi yake lenyewe pasipo kushurutishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *