Home > Featured_Slider > RC MAKONDA ATOA MILIONI 10 KWA KAMPUNI YA MSAMA AUCTION MART KUSAIDIA KUTOKOMEZA UHARAMIA WA KAZI SANAA

RC MAKONDA ATOA MILIONI 10 KWA KAMPUNI YA MSAMA AUCTION MART KUSAIDIA KUTOKOMEZA UHARAMIA WA KAZI SANAA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda ametoa Shilingi Milioni 10 za Kitanzania kwa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart inayosimamia zoezi la kutokomeza kazi feki za sanaa nchini.
Kiasi hicho cha Pesa kimetolewa katika Kampuni hiyo ya Msama ili kuendesha vizuri mapambano dhidi ya wanaodurufu kazi hizo sehemu zote za jiji la Dar.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa Kampuni hiyo inamshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kufanya jambo kubwa na la mfano ambalo hakulitegemea.
“Sikutegemea kuona kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anawapenda Wasanii, baada ya kuniita na kuniambia kuwa kazi ninayoifanya ya kupigania haki za Wasanii ni nzuri”, amesema Msama.”Ameniita amenimbia kazi inaenda vizuri, kwani amejaribu kupita maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar wala haoni Kompyuta, CD Feki na ameona kila CD anayoishika ina Stika ya TRA”, ameongeza Msama
Aidha, Msama ameendelea kusisitiza kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanafanya biashara yakuuza Kazi Feki za Sanaa waache kwa kutafuta kazi zakufanya.Pia amewaasa Wananchi kununua Filamu zenye Stika ya TRA inayong’aa vizuri, kwani watapofanya hivyo Wasanii hao watanufaika na kazi zao pamoja na kulipa Kodi kwa manufaa ya Taifa.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart, Bw. Alex Msama akizungumza na Wanahabari mapema jana jijini Dar,akieleza taarifa ya Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda kuongeza nguvu katika suala zima la kupambana na uharamia wa kazi sanaa hapa nchini,ambapo Mh Makonda amechangia milioni 10 kwa kampuni ya Msama Auction Mart ambayo inasimamia shughuli hizo za kupambana na Maharamia hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *