Home > Featured_Slider > NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA VIWANDA AKUTANA NA WAZIRI WA UWEKEZAJI JORDAN

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA VIWANDA AKUTANA NA WAZIRI WA UWEKEZAJI JORDAN

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  amekutana na Mhe. Muhannad Shehadeh, Waziri wa Nchi anaeshughulikia Uwekezaji kutoka   Jordan ambaye ameambatana na wafanyabiashara 40 kwa ajili ya kuangalia fursa za biashara na uwekezaji nchini.
Katika kikao hicho Mheshimiwa Naibu Waziri ameishukuru nchi ya Jordan kwa kuendelea kuwa na ushirikiano mzuri wa kisiasa na kiuchumi. Alimshukuru Mheshimiwa Waziri wa Jordan kwa kuongoza ujumbe huo mkubwa wa wafanyabiashara na alieleza kuwa ni imani yake wakati wa mkutano wa pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania walioletwa pamoja na TCCIA watapata fursa ya kushirikiana kwenye sekta mbalimbali za uwekezaji.

Nwaziri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *