Home > Featured_Slider > MWENYEKITI WA UVCCM NDG KHERI JAMES AFANYA ZIARA KWENYE VYOMBO VYA HABARI VYA CHAMA (CCM)

MWENYEKITI WA UVCCM NDG KHERI JAMES AFANYA ZIARA KWENYE VYOMBO VYA HABARI VYA CHAMA (CCM)

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndugu Kheri James afanya ziara kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi kujionea namna vinavyofanya kazi na kujua changamoto zao ikiwa sehemu ya kuimarisha mahusiano mema kati ya vyombo hivyo na UVCCM.

Kheri James alianza ziara hiyo kwenye gazeti la Uhuru na kisha kumalizia Radio Uhuru ambapo alijionea namna vinavyofanya kazi na kujionea changamoto kubwa zinazowakabili na kuwaahidi kuwa sauti zao kwenye vikao vya maamuzi.

Mwenyekiti Kheri aliviomba vyombo hivyo kuandika zaidi habari za vijana zitakazokuwa msaada kwa Vijana wote nchini na kuwasihi viongozi wa Radio Uhuru kuanzisha kipindi maalum kwa ajili ya Vijana wa Tanzania, hicho kipindi kitakuwa sauti ya Vijana na daraja kati ya Vijana na Serikal.

Ziara hiyo ambayo imefanyika Leo Jumanne Desemba 26, 2017, Mwenyekiti Kheri James aliambatana na Kaimu Katibu Idara ya Organaizesheni, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Mohammed Abdallah, Kaimu Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndugu Jokate Mwegelo pamoja na Maafisa wengine toka UVCCM Makao Makuu.

Imetolewa na,

*Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi

*UVCCM Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *