Home > Featured_Slider > NUKUU ZA ALIYOYASEMA KAIMU KATIBU MKUU WA UVCCM SHAKA HAMDU SHAKA KATA YA MUDIDA SINGIDA KASKAZINI

NUKUU ZA ALIYOYASEMA KAIMU KATIBU MKUU WA UVCCM SHAKA HAMDU SHAKA KATA YA MUDIDA SINGIDA KASKAZINI

Nukuu ya yaliyosemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka katika Kata ya Mudida Singida Kaskazini.

“Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kukubali ukweli na akiri yanayotekelezwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli yamevavutia na kuwapa matumaini mapya wananchi na kusababisha baadhi ya vigogo wa kisiasa kuanza kuupuza na kuukumbia upinzani”  Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini

“Mbowe asipotanabahi, kufanya tafakuri ya kina na uchambuzi makini wa kisiasa , chama hicho kitamfia mikononi mwake kwa sabahu kinaoonekana kumshinda.” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

“Siku zote katika maisha ukweli hauwezi kuzibwa na maneno ya mtu au kikundi kwani ukweli unafanana na miale ya jua na hivyo kamwe jua halitaweza kukingwa na kivuli cha binadamu.” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

“Amekuwa akijaribu kila wakati kujitutumua kisiasa ili kutaka kuipakazia na kuionyesha jamii kama serikali ya awamu ya tano haijaleta mabadiliko ya msingi kiuchumi, kiajira na kidemomrasia” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

“Mbowe aache ubishi badala yake awenjasiri na kukiri kama Dk Magufuli amekubalika. Midhali watoto wake wanamkimbia nyumbani kwake atarajie siku moja atabaki na wajukuu pia iko siku wajukuu nao watasambaa. Watu wanayaona yanayofanywa na serikali na kuwaridhisha ” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

“Mbowe kusema kuwa uchumi umeporomoka, kuna ukandamizaji wa Uhuru wa habari na mawazo , maisha kuwa magumu, ufinyu wa demokrasia na baadhi ya wabunge wake kupewa adabu za kinidhamu bungeni, anaonyesha kiongozi huyo kuhemewa kisiasa na sasa anatapatapa.” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

“Uchumi wa Tanzania kwa mujibu takwimu IMF unakua kwa kasi ya ya asilimia 6.5 na kuwa nchi ya tatu nyuma ya Ghana huku Ethiopia ikiongoza kukua kwa uchumi wake kinyume kabisa na madai ya Mbowe”.

” Kila siku mtazamo na kazi yake kubwa ni kuichafua Serikali ilio madarakani, kumnanga Rais kwa mambo ya kupika, uzushi na unafiki , kuwavunja matumaini wananchi na kutaka kuwagawa “Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

“Hakuna ugumu wa maisha bali kuna ugumu wa kuzibwa mianya ya ukwepaji kodi, kukata mirija ya matapeli na wapigaji dili hivyo hakuna fedha za ubwete mitaani.” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

“Hakuna demokrasia isioheshimu utii wa sheria na kwamba mantiki na maana ya demokrasia, tafsiri yake si matusi ya viongozi wa chama kimoja dhidi ya wengine ,  kutukana na kudhalilisha wenzako au kuzima vipaza sauti bungeni ndiyo upana wa suala hilo.” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

“Uvccm tunamueleza Mbowe akae akijua jahazi analoliongoza linaonekana kwenda mrama na mambo si shwari tena. Baadhi ya mabaharia wake wanachupa ili kujinusuru asisubiri hadi jumba bovu limdondokee. Akubali matokeo na kukiri kuwa Dk Magufuli ni piku mpya katika siasa za Tanzania na Afrika”Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

” Siasa za kina Mbowe na Chadema hazina maono wala mashiko hivyo Mwanasiasa yeyote nguli, mwerevu , makini na anayejua kucheza karata za kisiasa hawezi kuendelea kubaki ndani ya chama hicho kwakuwa kimepauka na kupoteza haiba yake” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

” Chama chochote cha siasa ni taasisi kamili yenye kujiendesha kimwelekeo utokanao na dira yake, malengo na madhumuni yake ikiwemo kuongozwa kwa mujibu wa katiba, taratibu, kanuni na miongozo badala ya fikara au utashi wa mtu mmoja na vile anavyoona yeye iwe akatenda kama afanyayo Mbowe huko chadema ” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

“Wananchi puuzeni porojo za wapizani na endeleni kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi na kumchagua Justine Monko awe Mbunge wa Singida kaskazini ili ashirikiane na Rais Dkt Magufuli kufanya kazi ya kuleta maendeleo.” Shaka Hamdu Shaka Singida Kaskazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *